Dodoma FM
Dodoma FM
5 June 2025, 4:49 pm

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Samia Day yaliyofanyika katika Wilaya ya Bahi, Kata yaZanka, Mhe. Kasper amesema fedha hizo zimeboresha miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu na afya.
Na Anwary Shaban .
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kasper Mmuya amesema katika kipindi cha miaka minne cha Rais Samia Suluhu Hassan jumla ya bilioni 51, 868, 901.17 zilitolewa kwa Wilaya ya Bahi, Kata ya Zanka.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Samia Day yaliyofanyika katika Wilaya ya Bahi, Kata yaZanka, Mhe. Kasper amesema fedha hizo zimeboresha miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu na afya.

Kwa upande wake, Joyce Paul Manyanda AfisaUtumishi amempongeza Rais Samia Suluhu kwa uboreshaji wa miradi ya elimu, hususani ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Naye Mwenyekiti wa kata hiyo Bw. Shaban Hassan na wananchi wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uboreshaji wa miradi katika kata hiyo.