Dodoma FM

Wananchi Makang’wa waendelea kupatiwa elimu ya urasimishaji

5 June 2025, 4:02 pm

Picha ni wananchi wakipatiwa elimu ya urasimishaji wa ardhi .Picha na google.

Zoezi la urasimishaji imekuwa ni mikakati ya Serikali kuhakikisha Kila mwananchi anamiliki ardhi yake kihalali Kwa kupewa hati ya umiliki wa ardhi za mashamba Yao.

Na Victor Chigwada.                                             

Imeelezwa kuwa elimu ya urasimishaji wa ardhi imeendelea kutolewa Kwa wananchi wa Kata ya Makang’wa Wilaya ya Chamwino wakati wakiendelea kusubiri zoezi hilo kuanza rasmi katika Kata Yao

Diwani wa Kata hiyo Bw.Samweli Machilik ameeleza kuwa jamii nimuhimu kwenda na wakati Ili kuongeza thamani ya ardhi yao ambayo itageuka kuwa faida kubwa mbeleni.

Ameongeza kuwa mwitikio wa wananchi juu ya elimu ya urasimishaji imepokelewa vizuri na kutokana na mahudhurio ya watu wanao fika katika seminar hizo za urasimishaji

Aidha amewaomba wakazi wa makang’wa kuondoa usumbufu wa migogoro pindi zoezi hilo litakapo wafikia ndani ya Kata yao.

Amesema kuwa zoezi la urasimishaji na upimaji ardhi bado lipo Kata jirani ya Mlowa barabarani baada ya kutamatika huko ndipo litahamia Makang’wa

Naye mwenyekiti wa Kijiji Cha Chiona Bw.Vicenti Chilewa amekiri elimu hiyo imeendelea kutolewa katika Kijiji chake lengo ni kuwandaa kisaikolojia na kuepuka mizozo isiyo na lazima.

Amesema kuwa ni vyema Kila mwananchi kuhakikisha anaondokana na mgogoro wa mipaka ya maeneo yao ambayo yanaweza kuleta changamoto pindi zoezi hilo litakapo anza