Dodoma FM

Wakazi Chinyika wapongeza uboreshaji wa miundombinu

3 June 2025, 2:20 pm

Picha ni moja ya barabara za mtaa huo ambayo imechongwa.Picha na Husna Abdallah.

Wakazi hao wamesema zamani miundombinu ya barabara, huduma za muhimu za kijamii ikiwemo kituo cha afya, maji safi na salama, umeme ilikuwa changamoto.

Na Husna Abdallah.

Wakazi wa mtaa wa chinyika kata ya mkonze jijini dodoma wametoa pongezi zao kwa uongozi wa kata hiyo kwakuboresha miundombinu ya bara bara za mitaa  na huduma za kijamii.

Wakizungumza na taswira ya habari  wakazi hao wamesema zamani wakati wamehamia katika mtaa huo miundombinu ya barabara, huduma za muhimu za kijamii ikiwemo kituo cha afya, maji safi na salama, umeme ilikuwa changamoto kubwa  katika kupata huduma hizo kwa wakati huo.

Sauti za wananchi

Akitolea ufafanuzi suala hilo la huduma za kijamii katika mtaa wa chinyika kata ya mkonze mkoani dodoma  mwenyekiti wa mtaa huo bwana Kombo Ally kombo amesema wakati anaingia katika kipindi chake bara bara za mitaa hazikuwepo na huduma zingine za kijamii ikiwemo maji na umeme ilikuwa changamoto kubwa upatikanaji wake.

Sauti ya mwenyekiti.