Dodoma FM

Mavunde akabidhi jenereta shule ya msingi Bunge

3 June 2025, 1:48 pm

Picha ni wanafunzi wa shule ya msingi Bunge wakiwa pamoja na muheshimiwa mavunde na baadhi ya walimu na wadau.Picha na Lilian Leopord.

Umeme unapokatika shuleni hapo wanakosa maji lakini kupatikana kwa genereta hilo watakuwa wanapata huduma ya maji kwa muda wote.

Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde amekabidhi genereta la kisasa kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bunge lengo ikiwa ni kuendelea kuwasaidia wanafunzi hao kuendelea kupata huduma ya umeme na maji pindi umeme unapokatika.

Mavunde akizungumza baada ya mmakabidhiano amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidiii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Picha ni waziri Mavunde na baadhi ya wanafunzi na walimu wakati akikabidhi genereta hilo.Picha na Lilian Leopord.
Sauti ya Mh. Athony Mavunde

Aidha Mavunde amewataka walimu wa shule hiyo kujitoa na kuwasimamia wanafunzi kwa kuwafundisha ili wawasaidie wanafunzi hao waweze kupata ufaulu mkubwa katika shule hiyo.

Sauti ya Mh. Athony Mavunde

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya hiyo ya wasichana ya bunge wamesema genereta hilo litawapa uhakika wa kusoma nyakati za usiku pindi umeme utakapokatika.