Dodoma FM

Bahi kuja na marufuku kwa wajawazito kunywa pombe

13 May 2025, 4:09 pm

Picha ni Mratibu wa Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka FPCT Jane Mgidange akiongea na wananchi hao.Picha na Seleman Kodima.

Ikumbukwe kuwa Mradi wa Elimu Jumuishi unaotekelezwa na Kanisa FPCT katika mkoa wa Dodoma unatekelezwa kwenye wilaya mbili ambazo ni Dodoma na Bahi.

Na Seleman Kodima.

Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imesema ipo tayari kuwa na sheria ndogo ndogo za katazo la Akina mama wajawazito kunywa pombe katika Vilabu vya Pombe za kienyeji.

Hatua hiyo inakuja baada ya mradi wa Elimu Jumuishi unaotekelezwa na kanisa la FPCT kufanya Bonanza katika kijiji cha Bahi Makulu kata ya Mpamantwa huku lengo kuu likiwa ni  kutoa kwa Elimu kwa jamii kuhusu watoto wanaokutana na vikwazo vya kielimu wanatambuliwa na kujumuishwa kwenye nyanja za kijamii na kupata Fursa sawa.

Picha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi na Mnec Donard Mejetii akiongea na wananchi. Picha na Seleman Kodima.

Akitoa Elimu hiyo kwa wananchi walioshiriki Bonanza Hilo,Mratibu wa Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka FPCT Jane Mgidange amesema

Sauti ya Jane Mgidange.

Kutokana na Changamoto ,Mgeni Rasmi katika tukio hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi na Mnec Donard Mejetii amesema wapo tayari kuwa na sheria ndogo ndogo zenye kukutaza hali ya akina mama wajawazito kunywa pombe ili hali ni hatari kwa afya ya Mtoto ajaye.

Sauti ya Donard Mejetii

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mpamatwa Sospeter amesema hatua ya kufanyika kwa Bonanza hilo imesaidia kuhamasisha umuhimu wa Elimu jumuishi kwenye jamii yao.

Sauti ya Sospeter.

Katika Bonanza hilo lilihusisha Michezo mbalimbali  ikiwemo  Mpira wa Miguu ,Uvutaji wa kamba,kukimbiza kuku,Kukimbia na Magunia na utoaji wa Zawadi kwa makundi mbalimbali hasa washindi wa michezo hiyo ,watoto wenye ulemavu na Wazazi.