Dodoma FM
Dodoma FM
6 May 2025, 5:49 pm

Ikumbukwe barabara hiyo ilitangazwa kuweka kiwango cha lami na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John pombe Magufuli alipo kuwa akizindua ujenzi wa reli mwendo kasi kutoka Morogoro Hadi Makutupola.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa changamoto ya ubovu wa barabara ya Ihumwa huenda ukabaki stori baada ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mh.Antony Mavunde kusema kuwa tayari barabara hiyo imeshakabidhiwa TANROAD tayari kuanza kushughulikiwa
Mavunde amesema kuwa mpango huo utatekelezwa haraka iwezekanavyo kutokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa barabara zote zinazo unga SGR ziwekwe kiwango cha lami
Ameongeza kuwa baada ya barabara hiyo kuwa kwenye mpango Kwa muda mrefu lakini Sasa hatua imefikia pazuri hivyo ni suala la TANROAD kutafuta mkandarasi wa kujenga barabara hiyo Kwa kiwango cha lami
Aidha Mavunde ameongeza kuwa hapo awali kulikiw na mvutano kati ya TANROAD na TARULA ni nani mwenye kusimamia lakini tayari wamefikia makubaliano na TANROAD ambao wanashughulikia kupatikana Kwa mkandarasi
Nao baadhi ya wananchi wametoa ombi lao kwa Serikali na TANROAD kuhakikisha ujenzi huo unaanza mara moja kabla ya msimu wa masika kwani ifikapo nyakati hizo mawasiliano Huwa ni magumu