Dodoma FM
Dodoma FM
29 April 2025, 6:15 pm

licha ya kuwa bado tuko mwezi wa nne lakini tayari baadhi ya familia zimeanza kulala na njaa
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kijiji Cha Mlodaa Kata ya Mlowa barabarani Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuingilia kati ili kupunguza ongezeko la bei za vyakula kwani ni hatari Kwa wananchi wa Hali ya chini.
Bi Fatima Rahim ni mama mpambanaji katika uuzaji wa chakula anaeleza namna ambavyo wanaathilika na kupanda Kwa bei ya mahindi pamoja mchele
Hali inayo inawaumiza walaji pamoja na wafanyabiashara hii yote ni kutokana ukame ulio sababishwa na uhaba wa mvua
Naye Anna Malindo ameongeza kuwa hali ya kuongeza bei ya bidhaa za chakula inawa gharimu watafutaji wa hali ya chini na kushindwa kuendesha maisha
Mwenyekiti wa kijiji cha Mloda Ndg.Adam Philimini amekiri Moja ya maeneo yaliyo athilika na uhaba wa mvua ni Kijiji chake Cha Mloda hivyo ni vyema Serikali kuwasaidia mahindi ya bei nafuu
Philimini amesema kuwa licha ya kuwa bado tuko mwezi wa nne lakini tayari baadhi ya familia zimeanza kulala na njaa jamboa ambalo ni hatari Kwa miezi ya mbele