Dodoma FM
Dodoma FM
24 April 2025, 5:31 pm

Ujenzi wa shule hiyo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 500.
Wanafunzi 320 wa kata ya kidoka wilayani chemba mkoani dodoma, wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu zaidi ya km 14 kwa sikukufuata shule kata ya jirani .
Hapo awali wanafunzi hao walilazimika kutembea umbali mrefu kuifuata shule maeneo ya kambi ya nyasa hali iliyo hatarisha usalama wao.
Serikali imetatua changamoto hiyo ya shule kwa kujenga shule katika eneo hilo ambayo imegharimu zaidi ya shilingi milioni 500.
