Dodoma FM
Dodoma FM
16 April 2025, 6:05 pm

Taswira ya habari imepita mtaani kufahamu watachukua tahadhari gani juu ya sheria hiyo.
Na Lilian Leopord.
Katika zama za sasa ambapo mitandao ya kijamii inachukua nafasi kubwa katika maisha ya kila siku, wazazi wanakabiliwa na changamoto nyingi kuhusu jinsi ya kushughulikia picha na video za watoto wao zinazochapishwa mtandaoni.
Hivi karibu Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Willfred Willa kutoka makao makuu ya Polisi Dodoma, kitengo cha dawati la jinsia na ulinzi wa mtoto katika semina ya siku 14 iliyoandaliwa na mgodi wa madini wa GGML amesema kulingana na sheria ya makosa ya mtandaoni kifungu cha 23, sheria namba 14 ya mwaka 2022 inaeleza kuwa mtu haruhusiwi kuposti mtu bila lidhaa yake mtandaoni ikiwa kitapelekea unyanyasaji wa mtu husika.
Sheria hiyo pia inaeleza kuwa mtu akitiwa hatiani atalipia faini ya kiasi cha shilingi milioni tano au kufungwa jela miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Taswira ya habari imepita mtaani kufahamu watachukuwa tahadhari gani juu ya sheria hiyo.
Wakati mwingine, watoto wanaweza kukabiliwa na matarajio yasiyo halisi kutokana na jinsi wanavyoonyeshwa mtandaoni, jambo ambalo linaweza kuathiri maisha yao ya baadaye.
kwa ujumla inaelezwa kuwa kuna athari hasi mbalimbali za kuchapisha picha au video za mtoto katika mitandao ya kijamii kutokana Mtoto hana uwezo wa kuamua kama anataka kupostiwa au la na huwenda mtoto akikua asipende hizo kumbukumbu ziwe katika mtandao.