Dodoma FM

Mila, desturi zatajwa kuwa kikwazo kwa wanawake katika uchaguzi

14 April 2025, 6:14 pm

Picha ni Neema Ahmed Wakili Chama Cha Wanasheria Wanawake (TAWLA).Picha na Lilian Leopord.

Lengo la kuandaa warsha hiyo ni pamoja na kujadili fursa na chanagamoto za wanawake ili kukuza na kuendeleza ushirika.

Na Lilian Leopord.
Mila na desturi na majukumu ya kifamilia vimekuwa ni vikwazo kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi katika vyama vya msingi vya ushirika.

Hayo yamesemwa na Neema Ahmed Wakili Chama Cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), katika mafunzo ya Jukwaa la Wanawake yaliyofanyika mkoani Iringa katika ukumbi wa Maktaba, lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuongozi wanawake.

Sauti ya Neema Ahmed .

Kwa upande wake Willium Mseme, ambaye ni Meneja Miradi Chama Kikuu Cha Ushirika amesema lengo la kuandaa warsha hiyo ni pamoja na kujadili fursa na chanagamoto za wanawake ili kukuza na kuendeleza ushirika.

Sauti ya Willium Mseme,

Baadhi ya wanawake walioshiriki mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo na yatakwenda kuwaletea usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi na kuondoa mfumo dume katika vyama vyao.

Sauti za baadhi ya wanawake