Dodoma FM

Mwenyekiti wa kitongoji adaiwa kumshambulia mwananchi

8 April 2025, 5:58 pm

Picha ni jeraha katika eneo la kichwa cha kijana huyo anae dai kushambuliwa na mwenyekiti huyo.Picha na Kitana Hamis.

Huku chanzo ikidaiwa kuwa niutani ulipelekea kiongozi huyo na vijana wengine wawili kumshumbulia na kumsababishia majeraha sehemu ya kichwani na mikononi.

Na Kitana Hamis.
Kijana aliyefamika kwa Jina la Abdalla Omary Said, Mwenye Umri wa miaka 30, mkazi wa Magugu,Wilayani Babati Mkoani Manyara amedaiwa kushambuliwa na Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Warangi (B) Kijiji Cha Magugu Wilayani Babati Mkoani Manyara.

Huku chanzo ikidaiwa kuwa niutani ulipelekea kiongozi huyo na vijana wengine wawili kumshumbulia na kumsababishia majeraha sehemu ya kichwani na mikononi Kwa mujibu wa maelezo.

kijana Omary,amesema tukio hilo lilitokea April 3, 2025 katika Kitongoji Cha Warangi (B) Ngarenaro, kijiji cha Magugu huku akimtuhumu Mwenyekiti wa Kitongoji cha Warangi B, Brayson Mushi akiwa na vijana wawili kumjeruhi baada ya Kijana huyokumtania kiongozi huyo.

Sauti za wananchi.