

7 April 2025, 5:18 pm
Miradi hiyo ni mradi wa barabara ya lami inayounganisha kata hiyo na Ipagala, zahanati ya Mpamaa, Shule ya Sekondari miyuji, na sule ya msingi mlimwa C.
Na Alfred Bulahya.
Kamati ya siasa kata ya Miyuji ikiongozwa na Diwani wa kata hiyo imefanya ziara ya kutembelea miradi 4 iliyojengwa ndani ya kata hiyo katika kipindi cha miaka 5 ya serikali ya awamu ya sita.
Akiongea baada ya kukamilisha ziara hiyo diwani wa kata hiyo Bi Beautice Ngelangela amesema kukamilika kwa miradi hiyo kumepunguza changamoto za kiafya, usafiri na elimu zilizokuwa zikiwakabili wananchi wa kata hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mpamaa amesema kwa sasa wanahudumia wagonjwa wengi ikilinganishwa na hapo awali huku wakuu wa Shule za Mlima C na Miyuji wakieleza namna itakavyoongeza ufaulu.
Wenyeviti wa Mitaa ya Miyuji Propa na Mpamaa wakaeleza furaha yao kutokana na miradi hiyo mikubwa kujengwa ndani ya mitaa yao.
Wananchi nao wanasema kuhusu usafiri, na huduma za Afya hali ni shwari kwa sasa.