Dodoma FM

Wakazi wa Mondela waiomba serikali kuboresha upatikanaji wa dawa

2 April 2025, 5:43 pm

Licha ya kuwa na bima ya afya ya NHIF lakini changamoto kubwa imekuwa ni kukosekana dawa na kuandikiwa kwenda kununua maduka binafsi.Picha na Google.

Itakumbukwa kuwa Machi 25 mwaka huu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa akiwa mkoani Kilimanjaro amepiga marufuku tabia ya waganga katika hospitali za serikali kuwaandikia wagonjwa dawa na kuwaelekeza kununua dawa hizo katika maduka ya dawa ya watu binafsi wakati serikali imetoa dawa za kutosha kwenye zahati, vituo vya afya na hospitali za wilaya.

Na Victor Chigwada.
Licha ya kukosekana kwa huduma ya zahanati kijiji cha Mondomela Wilaya ya Chamwino wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali kuhakikisha wanaboresha huduma ya upatikanaji wa dawa kupitia mfuko wa bima ya afya ya Taifa (NHIF).

Aidha wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema licha ya kuwa na bima ya afya ya NHIF lakini changamoto kubwa imekuwa ni kukosekana dawa na kuandikiwa kwenda kununua maduka binafsi.

Sauti za wananchi.

Aidha wameongeza kuwa kitendo cha watoa huduma kutoa maelekezo ya wapi mgonjwa akanunue dawa zinazohitajika imekuwa ikiwatia shaka kama kuna ubiya wa watumishio wa afya na wauzaji wa maduka hayo.

Sauti za wananchi.

Bw.Mathiasi Mele ni Diwani wa Kata ya Chinuguli amekiri kuwepo kwa malalamiko mengi juu ya upataji wa huduma za dawa kupitia bima ya afya na kuiomba Serikali kuongeza bajeti ya dawa.

Sauti ya Bw.Mathiasi Mele.