

1 April 2025, 6:25 pm
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), linawataka Watanzania kuanza kubadili mtazamo na kuziona taka kama fursa ya kuzirejeleza na kupata bidhaa mbalimbali na kujikomboa kiuchumi.
Na Mariam Kasawa.
Mamlaka za serikali za mitaa na halmashauri za wilaya nchini kote zimetakiwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu na kutambua kuwa taka ni fursa.
Jamii imekuwa na uelewa mdogo juu ya fursa inayopatikana katika taka ambazo nyingi huishia kurundikwa mahali pamoja au kuzagaa mtaani hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira.
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira mh. Khamis Hamza Khamis amelitaka baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira kuhakikisha elimu ya fursa zitokanazo na taka inawafikia wananchi mbalimbali na wananufaika .
Aidha amesema taka nyingi zimekuwa zikirundikwa na kusababisha uchafu na harufu mbaya mitaani .