Dodoma FM

BMH yafanya upasuaji wa jicho kwa njia ya matundu madogo

13 March 2025, 4:50 pm

Mpaka kufikia leo wamefanikiwa kuona wagonjwa 1020 katika magonjwa mbalimbali ya macho hospitali hapo. Picha na Benjamin Mkapa.

“Jambo ambalo tunajivunia ni kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya macho kwa njia ya upasua(Operation) wa matundu madogo ili kuondoa mtoto wa jicho.

Na. mwandishi wetu.
Hospitali ya Benjamin Mkapa imekuwa Hospitali ya kwanza katika sekta ya Umma kwa kufanya upasuaji (Operation) kwa njia ya matundu madogo.

Mkuu wa Idara Dkt. Jacinta Feksi amesema mpaka kufikia leo wameona wagonjwa 1020 katika magonjwa mbalimbali ya macho.

Ameongeza kuwa njia hii inafaida kubwa kwa mgonjwa kiuchumi na kiafya

“Hospitali ya Benjamin Mkapa itatoa matibabu haya kwa gharama ndogo ukilinganisha na maeneo mengine, hata hivyo njia hii humsaidia mgonjwa kupona marabaada ya upasuaji kufanyika na mgonjwa huruhusiwa siku hiyo hiyo” amesema Dkt.

Kwa upandewake Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho na mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dodoma Frank Sandi ameeleza ushirikiano wa madaktari Bingwa wa macho kutoka marekani (Morani) ni wa muda mrefu unazaidi ya miaka tisa sasa.

Aidha kiongozi wa Msafara wa Madaktari Bingwa wa Macho Morani Dkt. Jeff Pettey amesema ni fahari kuwepo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na kuona jinsi wataalamu wanavyo endelea kuwahudumia wananchi.