Dodoma FM

Jamii za wafugaji zatakiwa kusomesha watoto bila kubagua jinsia

13 March 2025, 3:46 pm

Picha ni kiongozi wa jamii ya kimasai Ole Parikei akiongea wakati wa sherehe ya kustaafu kwake.Picha na Kitana Hamis.

Laigwanani ni lazima astaafu unapofika umri wa kuustaafu na kubaki kama mshauri kwenye jamii hiyo.

Na Kitana Hamis.
Jamii imetakiwa kupeleka watoto shule wa jinsia zote bila kubagua.

Akizungumza na Dodoma tv wakati wa Kustaafu kwake kiongozi wa jamii ya kimasai Ole Parikei amesema ameihudumia Jamii hio kwa Miaka 64 nakuwauganisha na watu Wengine sambamba na kutatua Changamoto Mbali mbali ikiwemo Migogoro ya Aridhi huku akiwa Mstari wa Mbeli kuitaka Jamii hiyo kusomesha Watoto bila Ubaguzi wa Kijinsia.

Ole Parikea anasema yeye alisisitiza Zaidi Jamii ya kimasai Kuacha ubaguzi na mila kandamizi ikiwemo mila ya kutowamilikisha Aridhi Mtoto wa kike.

Sauti ya Ole Parikea .
Picha ni viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai wakiwa katika sherehe hiyo. Picha na Kitana Hamis.

Meshaki sasikari kiongozi wa mila akizungumzia kustafu kwa kiongozi huyo anaeleza kuwa kwa mujibu wa uongozi wa kabila la masai Laigwanani ni lazima astaafu unapofika umri wa kuustaafu na kubaki kama mshauri kwenye jamii hiyo.

Sauti ya Meshaki sasikari .

Kwaupande wa Familia ya Ole Parikei wakizungumzia nafasi ya mzee Huyo ambaye kwahivisasa nikikongwe wanasema amekuwa namsaada Mkubwa kwa Familia na jamii ya masai kwa ujumla.

Sauti za wana familia.