

11 March 2025, 1:15 pm
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unawafikia asilimia 8 ya Watanzania huku vituo vya afya vilivyosaijiliwa ambavyo vinalipwa na NHIF ni 10,004 nchi nzima.
Na Alfred Bulahya.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanikiwa kupunguza muda wa kuchakata madai ya watoa huduma za afya kutoka siku 120 hadi siku 45.
Hayo yamebainishwa Machi 10, 2025 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Mfuko huo ndani ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita ikiwa ni programu inayoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO.
Dkt. Irene ameeleza kuwa, hapo awali uchakati wa madai ulianzia kwa kujaza fomu ndipo mchakato wa NHIF uanze, kwani kwa sasa NHIF inatumia mfumo uitwao “Online Claim System” wenye uwezo wa kuchakata madai kwa haraka na kuondoa viashiria vyote vya udanganyifu.