Dodoma FM

Royal tour, amazing Tanzania zaongeza idadi ya watalii nchini

11 March 2025, 12:58 pm

Julai 2021 hadi Februari 2025 , watalii wapatao milioni 2.9 wametembelea vivutio vya utalii ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.Picha na Maelezo.

Mapato ya shilingi bilioni 693.959 yamekusanywa na kuingia katika Mfuko Mkuu wa Serikali.

Na Alfred Bulahya.
Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro(NCAA) imesema takwimu zinazoonesha kuwa juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia filamu za Royal Tour na Amaizing Tanzania zimechangia kutangaza nchi na kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea vivutio vya utalii nchini.

Ambapo katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2025 , watalii wapatao milioni 2.9 wametembelea vivutio vya utalii ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Watalii wapatao milioni 2.9 wametembelea vivutio vya utalii. Picha na Maelezo.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo Machi 10,2025 na Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro Dkt.Elirehema Doriye wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na muelekeo wa Mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.

Dkt.Elirehema amesema kuwa katika kipindi hicho mapato ya shilingi bilioni 693.959 yamekusanywa na kuingia katika Mfuko Mkuu wa Serikali.

Sauti ya Dkt.Elirehema Doriye .