

11 March 2025, 12:36 pm
Siku ya wanawake duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza siku hii kama siku ya kukumbusha dunia kuhusu haki za wanawake. Tangu wakati huo, siku hii imekuwa ikitumiwa kama fursa ya kuhamasisha harakati za usawa wa kijinsia duniani kote.
Na Lilian Leopord.
Siku ya Wanawake Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi, ni fursa muhimu ya kuangazia haki za wanawake na usawa wa kijinsia.
Katika jamii nyingi, kazi za ujenzi zimekuwa zikichukuliwa kama kazi za wanaume pekee. Hata hivyo kuna wanawake wengi wanaoshiriki katika sekta hii, wakifanya kazi kama wauzaji wa vifaa vya ujenzi. Ivon Matemu ambaye ni Msimamizi wa Kaizari Bulding Materials ameeleza ni kwa namna gani ameweza kufanya kazi hiyo.
Ameongeza kuwa anajivunia sana kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na wanawake wenzake, na amewataka wanawake kutokubagua kazi yoyote ile kwani hakuna kazi iliyotengwa kwa ajili ya wanaume pekee.
Consolatha Kalori ni Msaidizi wa Kaizari Building Materials amebainisha mafanikio aliyoyapata kutokana na kazi hii.
Licha ya mafanikio, Kalori amebainisha changamoto mbalimbali anazokumbana nazo katika kazi yake.