

4 March 2025, 12:00 pm
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni Wakala wa Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Na Alfred Bulahya.
Serikali kupitia mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi VETA imewawezesha wafungwa wapatao 214 kwa kuwapatia vyeti vya utambuzi juu ya ujuzi mbalimbali.
Hayo yamebainishwa Marchi 3, 2025 na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka hyo CPA. Anthony Kasore, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mafanikio ya mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.
Mbali na hilo VETA pia imeweza kuwatambua mafundi waliopo mtaani wasiokuwa na Taaluma ya ujuzi husika.
Aidha amesema Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024, Serikali imekamilisha ujenzi wa vyuo 33 vya ufundi stadi, 29 vikiwa vya wilaya na vinne (4) vya Mkoa, kwa gharama ya Shilingi Bilioni 94.5.
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni Wakala wa Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Sura ya 82 ikiwa na majukumu ya utoaji, ugharamiaji, uratibu na ukuzaji wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini.