

26 February 2025, 5:30 pm
Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi imepelekea wanafunzi kukaa Kwa kubanana kwani baadhi Yao wanalazimika kukaa zaidi ya wanafunzi sabini katika chumba kimoja.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa Pomoja na kufanikiwa kuandikisha watoto wengi wa darasa la kwanza lakini mafanikio hayo yamegeuka kuwa changamoto shule ya msingi Dabalo.
Wananchi wa kijiji cha Dabalo wameiomba Serikali kutatua changamoto hiyo kwani kuja na wazo la elimu bure lilihitaji na kuongeza nguvu ya kuongeza vyumba vya madarasa.
Ili kukubaliana na wimbi la uandikishwaji wa watoto ambapo hapo awali baadhi ya watoto walikosa fursa ya kusoma kutokana na wazazi kuogopa gharama za kusomesha.
Diwani wa Kata ya Dabalo Wilaya ya Chamwino Ndug.Omary Kiguna amekiri uwepo wa changamoto hiyo ambayo inapelekea idadi kubwa katika chumba kimoja.
Ameongeza kuwa changamoto hiyo siyo msingi tu bali ni pamoja na sekondari ya Dabalo nayo ikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi.