Dodoma FM

Mtaa wa changanyikeni Miyuji wageuzwa dampo la Taka

20 February 2025, 6:02 pm

Picha ni takataka zikiwa zimekusanywa kwenye makazi .Picha na Noah Patrick.

Halmashauri ya jiji la Dodoma imeomba kusaidia kutatua kero ya taka katika eneo hili ili wananchi waweze kuepukana na mrudikano wa taka pamoja na hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko.

Na Mariam Kasawa.
Wakazi wa mtaa wa Changanyikeni kata ya Miyuji Jijini Dodoma wamelalamikia kuzagaa kwa taka ovyo kutokana na kukosa utaratibu wa kukusanya taka katika eneo hilo.

Nimetembelea katika eneo hilo na kuona taka zilivyo zagaa ovyo mitaani wakazi wa eneo hili wanadai kwamba taka nyingi zinatupwa nyakati za usiku kwani baadhi ya watu hukodi bodaboda na kupakia mifuko ya taka kisha kuitupa katika maeneo ya wazi.

Picha ni furushi la taka ambalo limetupwa katika eneo la wazi eneo ambalo sio rasmi.Picha na Noah Patrick.

Si eneo hili peke linalo weka taka ovyo bali mitaa ya jirani pia wamegeuza mtaa huu kuwa dampo lao la kurushia mifuko yao ya taka.

Balozi wa mtaa wa changanyikeni na balozi wa mtaa wa St. Gemma wao wanaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi ili mzabuni wa kukusanya taka anapo tokea asikate tamaa kutokana na wanachi kushindwa kulipa ada ya taka.