

18 February 2025, 7:43 pm
Dira ya mpango huu ni kuhakikisha watoto wote nchini Tanzania wanaweza kusoma na kuhesabu kufikia umri wa miaka 10.
Na Seleman Kodima.
Wakuu wa shule na walimu wa masomo katika shule 265 za msingi katika mikoa 11 hapa nchini wamepokea jumla ya shilingi 401 milioni kama bonasi ya utendajikazi kupitia mradi kiufunza.
Rehema kalinga ni Mwalimu wa shule ya Msingi Dodoma Makulu yeye ni miongoni mwa walimu waliofaidika na bonasi hizo kupitia mradi wa kiufunza unaotekelezwa na taasisi ya Twaweza katika mikoa 11 hapa nchini.
Hali ya kujifunza na kuongeza uelewa wa kkk 3 kwa wanafunzi wa darasa la kwanza ,la pili na la tatu ni miongoni mwa malengo makuu ambapo mwalimu huyu amefaidika na motisha zinazotolewa na mradi huo ,ambapo matokoe yake yameongeza morali na ukaribu kwa wanafunzi.
Motisha hizi zimekuwa na manufai gani kwa shule za Msingi hasa Dodoma Makulu,Amon Challo ni Mwl mkuu katika shule hiyo anabainisha miaka mitatu ya mapinduzi ya bakishihi kwa walimu na hali ya uelewa ya waanafunzi.
Je kiufunza ni nin na shule zinanufaikaje na mradi huo,Aidani EYakuzE ni mkurungezi MTENDAJI WA wa taasisi ya TWAWEZA anabainisha zaidi.
Shule 265 zilizopo katika mpango huu zilichaguliwa kutoka katika wilaya zenye utendaji duni zaidi nchini Tanzania, kulingana na data ya tathmini ya Kitaifa ya Darasa la Nne.