Dodoma FM

Serikali yakamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 1,365.87

17 February 2025, 6:13 pm

ushiriki wa wakandarasi wazawa kwenye kazi za Ujenzi, uko chini kwani katika kipindi cha miaka sita hadi leo jumla ya miradi 21 ilikuwa chini ya wazawa huku 96 ikienda kwa Wageni.Picha na Alfred Bulahya.

Serikali imepanga Kutenga asilimia kumi (10%) ya bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya Miradi ya mafunzo kwa vitendo kwa Makandarasi Wazawa.

Na Alfred Bulahya.
Serikali kupitiwa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 1,365.87 kwa kiwango cha lami huku kilometa 2,031.11 zimeendelea kujengwa kwa kiwango cha lami katika maeneo mbalimbali nchini.

Ujenzi huo umekamilika Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita kuanzia mwaka 2021 hadi Februari 2025, ikiwa ni mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu kutoka TANROADS ndugu Efatha Mlavi ameeleza mafanikio hayo.

Pamoja na mafanikio hayo Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imesema ushiriki wa wakandarasi wazawa kwenye kazi za Ujenzi, uko chini kwani katika kipindi cha miaka sita hadi leo jumla ya miradi 21 ilikuwa chini ya wazawa huku 96 ikienda kwa Wageni.

Aidha imepanga Kutenga asilimia kumi (10%) ya bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya Miradi ya mafunzo kwa vitendo kwa Makandarasi Wazawa ili kuongeza ushiriki.

Katika hatua Nyingine Msemaji mkuu wa Serikali amezitaka Taasisi zote za serikali kuhakikisha zinatoa taarifa za miradi ya maendeleo iliyofanya katika kipindi cha Miaka 4 serikali ya awamu ya 6.