

12 February 2025, 4:30 pm
Inaelezwa kuwa ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika mara kwa mara na kupelekea madhara makubwa kwenye jamii.
Na Kitana Hamis.
Wananchi Wilayani Kiteto mkoani Manyara wameeleza sababu zinazo pelekea kuvunjika kwa ndoa Mara kwa mara.
Baadhi ya Wananchi Wilayani Kiteto wameeleza sababu mbali mbali Juu ya kuvujika kwa ndoa hizo ambapo wanasema Wazee wa zamani walikuwa nauvumilivu lakini karne hii watu hawana uvumilivu Jambo dogo Sana anaweza kuvunja ndoa Ndoa nyinge zinavunjika kwa sababu nyingi mtu anaoa mtu ambaye sio changuo lake anafosiwa kuoa kwavile amesha fikia umri wa Kuolewa au kuoa kutokana na Ndugu jamaa marafiki walio mzunguka .
Nao Viongozi wa dini ya kiislam wilayani Kiteto wameeleza sababu za kuvunjika kwa ndoa hizo huku wakiwasihi jamii kufuata Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 .