

11 February 2025, 6:14 pm
Mafunzo ya waandishi wa habari katika radio za kijamii yamendaliwa na mtandao wa radio jamii,serikali ya mkoa wa kagera pamoja na wizara ya afya ambapo yanafanyika siku 3 kuanzia tarehe 10 ,12,2025 katika manispaa ya Bukoba.
Na Benard Filbert.
Waandishi wa vyombo vya habari vilivyopo kwenye mtandao wa radio za kijamii(TADIO wametakiwa kuendelea kuripoti na kutoa elimu sahihi kwa jamii kuhusu Ugonjwa wa MABURG.
Wito huo umetolewa na Kaimu Afisa Afya mkoa wa Kagera Salum Kimbau wakati akiwasilisha mada mbalimbali katika mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa ELCT BUKOBA kwa waandishi wa habari wa radio za kijamii.
Amesema waandishi wahabari katika radio za kijamii wananafasi kubwa katika maeneo yao hivyo ni vyema wakatumia kalamu zao kuhakikisha wanaielimisha jamii kuhusu magonjwa ya mlipuko ikiwepo Ugonjwa wa MABURG.
Ameongeza kuwa kwa siku 3 ambazo mafunzo hayo yanafanyika waandishi hao watapata nafasi ya kujifunza vitu muhimu kwa ajili ya kuongeza uelewa kwa jamii juu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Radio za kijamii TADIO nchini John Baptist Mutesasira amewapongeza waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo huku akiwataka waandishi hao kwenda kubadilisha mitazamo hasi iliyopo kwenye jamii kuhusu magonjwa ya mlipuko ikiwepo Maburg.
Aidha amesema ni vyema waandishi wa habari wakawa na uelewa pamoja na elimu kuhusu magonjwa ya mlipuko kwani wao wamekuwa wakiaminiwa na jamii kwa kiwango kikubwa katika maeneo yao.
Naye Mtaalamu wa mabadiliko ya Tabia katika jamii kutoka shirika la UNICEF Dokta Chikondi Khangamwa ameipongeza TADIO kwa kuandaa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari radio za kijamii ili kuwaongezea uelewa wa namna yakuripoti habari zinazohusu magonjwa ya mlipuko kwani kwani wataleta tija katika jamii zao.
Mafunzo ya waandishi wa habari katika radio za kijamii yamendaliwa na mtandao wa radio jamii,serikali ya mkoa wa kagera pamoja na wizara ya afya ambapo yanafanyika siku 3 kuanzia tarehe 10 ,2,2025 katika manispaa ya Bukoba Ukumbi wa Hotel ya ELCT huku lengo kubwa ikiwa kuongeza uelewa kwa waandishi wa habari namna ya kuripoti na kutoa elimu katika jamii kuhusu Ugonjwa wa Maburg.