Dodoma FM

Madereva bodaboda 759 wafariki kati ya mwaka 2022 na 2024

11 February 2025, 5:41 pm

Picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo akiongea leo Bungeni Jijini Dodoma.Picha na Bunge .

Mbali na vifo vya madereva hao, Sillo amesema kuwa wananchi wa kawaida 283 pia wamefariki dunia kutokana na ajali za bodaboda katika kipindi hicho.

Na Lilian Leopord.
Jumla ya madereva bodaboda 759 wamefariki dunia kutokana na ajali kati ya mwaka ya 2022 na 2024.

Hayo, yamesemwa, Jumanne Februari 11, 2025, Bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Fatuma Hassan Toufiq.

Mbunge huyo aliuliza ni wananchi wangapi wamepoteza maisha kutokana na ajali za pikipiki kati ya mwaka 2022 na 2024.

Sauti ya Mh.Daniel Sillo.

Mbali na vifo vya madereva hao, Sillo amesema kuwa wananchi wa kawaida 283 pia wamefariki dunia kutokana na ajali za bodaboda katika kipindi hicho.

Sanjari na hayo, Sillo ameto wito kwa makamamda wa usalama barabarani kusimamia sheria za usalama barabarani na kuwataka watumiaji wa barabara ikiwemo madereva bodaboda na watembea kwa miguu kuzingatia sheria hizo.

Sauti ya Mh.Daniel Sillo.