

10 February 2025, 5:49 pm
Idadi kubwa ya wakazi wa eneo hili ni wafugaji wanakaa maeneo ya pembezoni ambapo ni vigumu kupata taarifa.
Na Kitana Hamis.
Wananchi wilayani Kiteto Mkoani Manyara waiomba serikali kuwajengea nyumba salama waathiriwa wa vitendo vya ukatili.
Wakizungumza na Dodoma Tv Wananchi hao wamesema Vitendo vya Kiukatili ikiwemo Ukeketaji Ulawiti Ubakaji na Vipingo umekidhiri hivyo kesi nyingi zimekuwa zikiharibika kutokana na Baadhi ya watuhumiwa kuwa Karibu na wathiriwa.
Dodoma Tv imemtafuta Mkuu wa Wilayani ya Kiteto Mh .Remidius Mwema ili kufahamu mpamgo wa serikali juu ya ujenzi wa nyumba salama kwa wananchi walio kumbwa na vitendo vya ukatili lakini hakuweza kuzumza kwa madai kuwa yupo kwenye kikao.
Naye mjume wa kamati ya Taifa ya kutokomeza yakutokomeza Ukatili wa Wanawake na Watoto Kiteto Joseph Kahaya anaeleza jitihada za Ujezi huo wa Nyumba Salama.
Mratibu wa shirika lisilo kuwa la Kiserikali Kiteto Legal aid ( KLHA) anaeleza Hali ya Ukatili huku akisema Kiteto inashika nafasi ya Pili kwa Vitendo vya Kiukatili.