

7 February 2025, 4:15 pm
Mradi huo unatarajia kunufaisha wakulima 27,600 nchi nzima, huku kila Halmashauri ikitarajiwa kupata visima kumi(10).
Na Mariam Kasawa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amemtaka Mkandarasi wa kuchimba visima vya umwagiliaji katika Mkoa huu, kuhakikisha kuwa anakamilisha mradi huo kwa wakati ili wakulima waweze kunufaika na uwekezaji ambao ni muendelezo wa jitihada za Serikali kukuza sekta ya kilimo pamoja na kuwainua Wakulima Kiuchumi.
Mhe. Senyamule ameyasema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya eneo kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha umwagiliaji liyofanyika katika Mtaa wa Chamwino kata ya Chihanga, Jijiini Dodoma.
Naye Meneja wa Umwagiliaji mkoa wa Dodoma, Mhandisi Oswald Urassa, amesema mradi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais ambapo unatarajiwa kunufaisha wakulima 27,600 nchi nzima, huku kila Halmashauri ikitarajiwa kupata visima kumi(10). Katika awamu ya kwanza vitachimbwa visima sabini(70), Mkoa wa Dodoma utapata visima sita (6) ambavyo vitachimbwa katika wilaya za Kondoa, Bahi, Kongwa, Chemba, Chamwino na Dodoma .