

7 February 2025, 3:34 pm
Mfumo wa stakabadhi wa Ghala umeendelea kuimarika zaidi kwani Msimu wa 2024/25.
Na Mariam Kasawa.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Seleman Jafo ametanganza ukoma wa msimu wa manunuzi ya mfumo wa stakabadhi wa Ghala Msimu wa 2024/25 na kuanza kwa msimu wa 2025/26.
Waziri Jafo ameyabainisha hayo Leo Februari 7 jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa Habari amesema Mfumo wa stakabadhi wa Ghala umeendelea kuimarika zaidi kwani Msimu wa 2024/25 jumla ya bidhaa 14 zilikusanywa na kuuzwa kupitia mfumo wa ghala na stakabadhi.
Hali ya thamani ya mazao imeongezeka pamoja na ushiriki wa wananchi umeongezeka na kuchangia Halmashauri ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka Bilioni 36 hadi Bilioni 87 huku Jumla ya 241 maghala yamepatiwa Leseni.