

6 February 2025, 3:10 pm
Prof. Abel Makubi amesema wanatamani sasa hospitali ya Benjamin Mkapa iwe hospitali ya taifa.
Na Mariam Kasawa.
Wananchi wametakiwa kuendelea kujitokeza na kupata huduma ya matibabu katika hospitali ya Benjamini Mkapa ambayo ni hospitali ya kibingwa .
Hayo yamesemwa na Spika wa bunge mstaafu ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa Mh Job ndugai katika ziara ya baadhi ya wabunge ambao walikaribisha kutembelea hospitalini hapo ambapo amesema hospitali hii ina huduma nyingi za kibingwa hivyo wananchi wa kanda ya kati na mikoa mingine wanakaribishwa kupata matibabu.
Katika kuadhimisha miaka 10 ya hospitali ya Benjamini mkapa akieleza mafanikio ya hospitali hiyo kwa wabunge walio tembelea hospitali hiyo mkurugenzi wa hospitali ya Benjamini Mkapa Prof. Abel Makubi amesema wanatamani sasa hospitali ya Benjamin Mkapa iwe hospitali ya taifa kutokana na kukidhi vigezo.
Nao baadhi ya wananchi ambao wapo hospitalini hapo kwaajili ya matibabu wanasema huduma zinazo patikana ni nzuri lakini wameiomba serikali itazame kwa upande wa gharama hasa kwa wale ambao hawana bima watibiwe hata kwa kudhaminiwa pale wanaposhindwa kumudu gharama za matibabu kwa haraka.