Dodoma FM

Wananchi wilayani Kiteto waeleza changamoto zao kilele wiki ya sheria

5 February 2025, 12:57 pm

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto Boniface Lemwita ambaye pia alikuwa Mgeni rasim katika kilele cha Mazimisho ya Sheria.Picha na Kitana Hamis.

Mashauri yanayokwenda kwa viongozi na yanashidwa kushughulikiwa mwisho siku yanakaa mda mrefu .

Na Kitana Hamis.
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto Boniface Lemwita ambaye pia alikuwa Mgeni rasim katika kilele cha Mazimisho ya Sheria wilayani Kiteto anasema Miongoni mwa Haki katika Mahakama nipamoja na kutolewa Hukumu Mahakama ya Wilaya.

Bw. Boniface anasema mwaka 2024 walibakia na mashauri miamoja (100) lakini walipokea Mashauri mia moja sitini na nane (168) yalisikilizwa Mashauri Miamoja Tisini na Mbili (192) na yakabaki Mashauri sabini na sita (76).

Nae Mkuu wa Wilayani ya Kiteto Remidius Mwema amesema ndani ya Wilaya ya Kiteto hakuna Mgogoro wa ardhi ambao hauna Majibu kwani kila Mgogoro unaofahamika wilayani humo tayari umeanza kufanyiwa kazi.

Wakiwasilisha hutuba mbali mbali ikiwemo Chama cha Mawakili Tanzania Teliesi na ya Mwendesha Mashtaka ya Serikali hapa wanasema kutakuwa na Mifumo imara yakisheria na yakitaasisi yatakayo Wezesha Haki kufikiwa kwa haraka na kwa Ufanisi .

Nao baadhi ya Wananchi wamesema changamoto za Kisheria zinazo wakumba wilayani humo ni ri Mashauri yanayokwenda kwa viongozi na yanashidwa kushughulikiwa mwisho siku yanakaa mda mrefu .