Dodoma FM

TRA kuwapunguzia kodi manusura janga la moto

27 January 2025, 6:23 pm

Picha ni tukio la moto lililo tokea jijini Dodoma hivi karibuni.Picha na Dodoma Tv.

TRA), mkoa wa Dodoma imesema itatumia sheria zilizopo kuwapatia unafuu wa kikodi wafanyabiashara walioathirika.

Na Seleman Kodima.
Ikiwa siku chache zimepita tangu takribani maduka 14 yaliyopo mtaa wa Kipande katikati ya jiji la Dodoma kuteketea kwa moto, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mkoa wa Dodoma imesema itatumia sheria zilizopo kuwapatia unafuu wa kikodi wafanyabiashara walioathirika na janga hilo.

Hayo yameelezwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Pendolake Elinisafi, leo Jijini Dodoma mara baada ya kuwatembelea wafanyabiashara hao kwa lengo la kuwapa pole na faraja katika kipindi hiki kigumu.

Amesema nguvu kubwa iliwekwa na wafanyabiashara hao hivyo kama serikali itakuwa pamoja nao mpaka pale watakapopata nguvu tena ya kuanza upya.

Maduka 14 yaliteketea kwa moto uliozuka asubuhi ya Januari 21, 2025 na kusababisha hasara na uharibifu wa mali, hali iliyosababisha taharuki miongoni mwa wafanyabiashara wa eneo hilo huku chanzo cha moto kikiwa bado hakijajulikana.