Ukarabati wa barabara warahisisha mawasiliano Majeleko
27 January 2025, 4:00 pm
Utekelezaji miradi ya kilomita ishirini na tano kwa kiwango cha changarawe imesaidia kuunganisha Vijiji hivyo.
Na Victor Chigwada.
Ukarabati wa miundombinu ya barabara kutoka wilunze mpaka manzilanzi na Majeleko umesaidia kuleta unafuu wa mawasiliano katika vijiji vya kata ya Majeleko.
Hayo yamethibishwa na Diwani wa Kata ya Majeleko Bw.musa Omari wakati akizungumza hali ya miundombinu katika kata hiyo ambapo amesema utekelezaji miradi ya kilomita ishirini na tano kwa kiwango cha changarawe imesaidia kuunganisha Vijiji hivyo.
Musa Omari ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kupitia kwa mbunge wao Mh.Deo Ndejembi kwa kufanikiwa kutoa miradi mingi ambayo imeambatana na utekelezaji wake.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mbelezungu Bw.George Mkung’huni amekiri kuwepo kwa unafuu miundombinu ya barabara baada ya kukamilka kwa matengenezo hayo.
Nao baadhi ya wananchi wamesema kuwa hapo awali barabara ilikuwa imejaa mashimo hali iliyopelekea changamoto kwa watumiaji.