Dodoma FM

Jeshi la Polisi Manyara lakamata pikipiki 80 zinazovunja sheria

24 January 2025, 1:55 pm

Picha ni Pikipiki zilizo kamatwa katika oparesheni hiyo. Picha na Kitana Hamis.

Makosa hayo nikutokuwa nakofia ngumu pamoja na Makosa Mengine.

Na Kitana Hamis.
Akizungumza kuhusu Operesheni hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara Ahmed Makarani amesisitiza kuwa Jeshi hilo litawachukulia hatua kali za Kisheria Madereva watakaokiuka Sheria za Usalama Barabarani na Operesheni hiyo itakuwa endelevu.

Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoani Manyara limefanikiwa Kukamata Pikipiki Takribani 80 zikiwa na Makosa Mbali mbali.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara Ahmed Makarani amesisitiza kuwa Jeshi hilo litawachukulia hatua kali za Kisheria Madereva watakao kiuka Sheria.Picha na kitana Hamis.

Makosa hayo nikutokuwa nakofia ngumu pamoja na Makosa Mengine,kwa Lengo la kudhibiti ajali na kuhakikisha Usalama wa Watumiaji wa Barabara Katika Mkoa huo.

Nao watumiaje wa vyombo vya Moto marufu kama Bodaboda wanasema kutokana na Operesheni hii iliyo fanyika itasaidia kupunguza makosa mbalimbali yanayo fanyika barabarani.