Dodoma FM
Serikali yaombwa kukamilisha ujenzi wa mitaro Mpwapwa
24 January 2025, 1:34 pm
Wamesema pindi mvua zinaponyesha Maji yanaingia kwenye Nyumba zao hali inayo hatarisha usalama wa wananchi.
Na Steven Noel.
Wananchi wa mtaa wa hazina kata ya Vig’hawe wilaya ya Mpwapwa wameiomba serikali imalizie ujenzi wa mitaro ya maji kwenye barabara inayojengwa toka hospitali Hadi namba thelathini kutokana na pindi mvua zinaponyesha Maji yanaingia kwenye Nyumba zao.