Dodoma FM

Vitongoji vitatu jijini Dodoma vyaililia serikali changamoto ya maji

23 January 2025, 6:06 pm

Wananchi hao wameiomba Serikali kutatua adha hiyo ya maji kwani imekuwa kero kwao.Picha na google.

Wakieleza namna ambavyo kukosekana kwa maji safi na salama kunavyo waathiri wananchi hao ,wananchi hao wameiomba Serikali kutatua adha hiyo.

Na Victor Chigwada.
Wananchi wa vitongoji vya Chidobwe,Kaunda na Liwangama Kolimba wameiomba Serikali kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Baadhi ya wananchi hao wameiomba Serikali kufuatilia mamlaka za maji ili kufahamu usimamizi wa rasilimali hiyo ili kujua njia gani sahihi ya kusimamia miradi ya maji chini ya wananchi.

Sauti za baadhi ya wananchi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa vitongoji hivyo vinavyo patikana katika kijiji cha Muungano Matonya Mtukamsihi amekiri uwepo wa changamoto hiyo ya maji safi na salama.

Sauti ya Mwenyekiti.