Wakulima watakiwa kuzingatia njia sahihi za kilimo
23 January 2025, 5:35 pm
Katika kuhakikisha wakulima wanazingatia msingi wa kilimo bora,shirika la Rikolto wameendelea kutoa Elimu wa wakulima kuhusu kilimo bora ,lishe na usawa kijinsia pamoja na usalama wa chakula.
Na Seleman Kodima.
Imeelezwa kuwa ili kuwa jamii yenye afya njema ipo haja wakulima kuzingatia kanuni na njia sahihi za kilimo ili kupata mazao yenye ubora na kuhakikisha uwepo wa usalama wa chakula.
Hili linajiri baada ya hivi karibu Taswira ya Habari kuzungumza na baadhi ya wakulima kutoka kijiji cha Manchali wilayani Chamwino kuhusu wanazingatiaje kilimo bora na usalama wa chakula ambapo baadhi yao wamesema njia mojawapo na kufatilia elimu wanayopewa na wataalamu wa kilimo kabla ya kulima zao lolote.
Maiko Ngubesi na Ayoub Mwendi ni wakulima kutoka kijiji cha Manchali wanasema ili kuzingatia kilimo bora na usalama wa chakula ni muhimu zaidi kutokosea kwa hatua yeyote ya kilimo ili kumlinda mlaji wa mwisho.
Je ni changamoto gani wanakukutanazo wakati wa utekelezaji wa kilimo bora na Usalama wa chakula,Eda Mwendi na Saimoni Mwalimu wanaeleza zaidi.
Lilian Mbilinyi ni Afisa kilimo,Biashara kutoka Shirika la Rikolto amesema zipo faida lukiki kwa mkulima iwapo atazingatia kilimo bora na usalama wa chakula hasa katika mnyororo wa thamani na kulinda mlaji wa chakula .
Kwa upande wake Afisa Ugani kutoka kijiji cha Manchali Ayoub Ramadhani amesema usalama wa chakula unahakikishia kaya kuwa salama kwenye upatikanaji wa chakula kwa mwaka mzima.