Serikali yarejesha tabasamu kwa wakazi wa Mlazo
16 January 2025, 3:44 pm
Pamoja na Kuhamasisha, kulinda na kurejesha Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuzingatia na mipango sahihi, ya kufikia maendeleo endelevu ya Afya ya Jamii.
Na Victor Chigwada.
Tabasamu limerejea kwa wananchi wa kijiji cha Mlazo wilayani chamwino baada ya serikali kuboresha huduma za afya kwa kusogea karibu huduma hizo.
Hayo yanajiri baada ya ujenzi wa zahanati kuanza katika Kijiji hicho ambapo kwa muda mrefu wananchi wa kijiji hicho walikuwa hawana zahanati na kulazimika kutembea umbali mrefu.
Wamesema hatua ya ujenzi huo itasaidia kupunguza changamoto hizo na kusaidia wananchi kupata huduma karibu.
Diwani wa Kata ya Ngh’ambaku Haruna Siego ameelezea namna huduma ya afya imeendelea kuimarika katika Kata hiyo ambapo sasa wameanza ujenzi wa zahanati mpya katika kijiji cha Mlazo.
Hatua ya ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Mlazo ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu hasa namba tatu katika Kuwa na jamii yenye afya bora na ustawi ambayo inachangia kikamilifu katika maendeleo binafsi na ya nchi.