Wananchi Dosidosi waharibu miundombinu ya maji
13 January 2025, 4:12 pm
Wananchi hao wameiomba serikali kufuatilia mabomba yaliyo katwa ili kutatua kero ya maji kijijini hapo.
Na Kitana Hamis.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Dosidosi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara Wamedaiwa Kuhujumu Miradi ya Maji wazaidi ya sh: milioni Mianne (400) kwa kukatakata mabomba ili maji yasitoke.
Baadhi ya Wananchi wanasema Ndoa zao zinakufa kwajili ya maji ambapo hulazimika kufuata maji umbali mrefu .
Dodoma fm imezungumza na Wazee wa kijiji ambapo wanaeleza namna hali iliyo kwa hivi sasa Wanasema hali nimbaya kwani wanashidwa kwenda Msikitini kwajili ya maji na namatumizi migine yanakwama kwani hulazimika kununua ndoo ya maji kwa shilingi 500 kila siku ili waweze kukidhi mahitaji yao.
Mwenye kiti wa kijiji cha Dosidosi Wilayani Kiteto amewaomba wananchi kuwa na uvumilivu huku akionya makundi ya watu wanao husishwa kukata mabomba ya maji kijijini hapo.
Nae Meneja wa Ruwasa Wilayani Kiteto ameeleza hasara ya uharibifu wa Mradi huo ulivyo haribiwa huku akiiomba Serikali ya Kijiji cha Dosidosi kutusaidia kuwabaini waharibifu wa miundombinu hiyo ili waweze kuchukuliwa hatua.