Wanaume jamii ya Masai watuhumiwa kuuza nyanda za malisho
8 January 2025, 2:44 pm
Maeneo ya malisho yanayodaiwa kuuzwa niyale yaliyo Tengwa kwa shughuli za Ufungaji.
Na Kitana Hamis.
Wanaume jamii ya Kifungaji masai Kiteto Watuhumiwa Kuuza Nyanda za Mlisho
Wakizungumza kwa hisia kali Baadhi ya Wanawake wa Jamii ya Kifungaji Masai wanasema Migogoro mingi ya Ardhi Kiteto inachangiwa na Waume zao haswa Jamii hio ambao wamekuwa wakiuza Ardhi katika Maeneo yao ya Malisho nakununua Mifugo ili hali wakijua hakuna maeneo mengine ya malisho badala yake huchangia Migogoro ya Ardhi.
Maeneo ya malisho yanayodaiwa kuuzwa niyale yaliyo Tengwa kwa shughuli za Ufungaji Mwenyekiti wa Maene hayo anasema Migogoro mingi ya Ardhi Kiteto unakuta mtu anauza Eneo lake la Kilimo alafu anaenda kununua Mifugo Hanang na Wilayani ya Mbulu huku zikija zinakufa na njaa namatokeo yake anaaza Kug’ag’ania tena eneo alilo uza ndomana Migogoro ya Ardhi baina ya Wafugaji na wakulima haishi.
Naye Afisa Tarafa ya Kibaya ameonya vikali juu ya Ukatili unavyo fanyika kwa Jamii hiyo ya kifungaji Masai ikiwemo kuozesha Watoto Wakiwa bado Wadogo.
Mkuu wa Wilayani ya kiteto Remidius Mwema ameeleza changamoto za migogoro ya ardhi kiteto nakutoa maelekezo Juu ya utatuzi wa Migogoro hio huku Paulina ngurumo kutoka Shirika la Kinapa akizungumza na Kinamama kuwa kunahaja ya kuazisha Vikundi vya Wanawake kwenye Vijiji Watakao linda Ardhi yao.