Dodoma FM

Wanawake Olboloti walia na janga la ubakaji

8 January 2025, 2:09 pm

Picha ni wanawake wa kijiji cha Olboloti kilichopo wilayani Chemba Mkoa wa Dodoma. Picha na Kitana Hamis.

Wanaohisiwa kufanya vitendo hivyo baadhi yao saba wamekamatwa na mmoja kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.

Na Kitana Hamis.
Wananchi wa kijiji cha Olboloti wilayani Chemba mkoani Dodoma wakiongea kwa jazba huku huzuni iliyojaa maumivu kueleza changamoto zinazowakabili hapo kijijini, baadhi ya akinamama wamepaza sauti zao huku wakiomba watumishi wa serikali kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao.

Kwa mujibu wa taarifa za mauaji kijijini hapo, jumla ya watu watatu wamepoteza maisha. Hata hivyo baada ya msako kwa kundi hilo la vijana maarufu kama MARONJOO wanaovizia akinamama wakati wakienda mashambani, kuchanja kuni hata gulioni huwafanyia vitendo vya kikatili kwa kuwabaka na kuwapa majeraha sehemu mbalimbali kwa kutumia vitu vyenye ncha kali.

Mmoja kati ya watu wanaohisiwa kuwa wahalifu akiwa amechomwa moto na wananchi wenye hasira kijijini hapo. Picha na Hamis Kitana.

Wananchi pia walilazimika kuvamia kituo cha polisi na kupiga mawe wakishinikiza watuhumiwa waachiwe ili wananchi wajichukulie sheria.

Kwa upande wake Mwenyekiiti wa Kijiji hicho cha Olboloti ameeleza kuwa tayari wameweka mikakati ya kupunguza uhalifu hapo kijijini.

Kamada wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabazi amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akiwataka wananchi hao kuwa na utamaduni wa kuripoti natukio hayo kabla ya madhara kujitokeza.