Utenganishaji wa taka unavyorahisisha uchakataji wa taka za plastiki
7 January 2025, 5:16 pm
Kama Halmashauri zitatambua aina na kiasi cha taka kinachozalishwa katika eneo lake ni rahisi kutenganisha taka hizo kwa kuyapa rangi tofauti tofauti mapipa au vizimba vinavyokusanya aina tofauti ya taka hizo.
Na Mariam Kasawa.
Vikundi vya ukusanyaji taka katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma vimetakiwa kufuata utaratibu wa kuhifadhi chupa za plastiki katika vifaa maalum vilivyo tolewa ili kutunza mazingira.
Katika kata ya Chamwino Jijini Dodoma wamebahatika kupata mradi wa majaribio wa uchakataji chupa za plastiki mradi ambao utawasaidia wakazi hao si kupunguza taka za plstiki mitaani bali hata kujipatia kipato.
Ugawaji wa vifaa vya kuhifadhia taka za plastiki katika vikundi vya ukusanyaji taka hususani katika kata ya Chamwino utasaidia zoezi la kukusanya chupa kuwa rahisi kutokana na kuhifadhiwa sehemu moja pamoja na kuzitenga chupa hizo na taka zingine kama anavyo eleza mwenyekiti wa vikundi vya usafi jiji la Dodoma Bw. Selemani Sanya.
Bi Perpetua Kasase muuguzi kutoka zahanati ya Chamwino anasema wamekuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa wateja na wagonjwa ikiwemo utaratibu wa kutupa chupa za plastiki katika vifaa maalum pamoja na kutenganisha taka.
Jamii inapaswa kuelewa juu ya faida za kutenganisha taka ambazo zina oza na zisizo oza na pia kutokana na aina za taka vijana kutoka vikundi vya usafi wao wanazungumziaje juu ya vifaa hivi vya kuhifadhia chupa za plastiki.
Kama Halmashauri zitatambua aina na kiasi cha taka kinachozalishwa katika eneo lake ni rahisi kutenganisha taka hizo kwa kuyapa rangi tofauti tofauti mapipa au vizimba vinavyokusanya aina tofauti ya taka hizo, hii itasaidia kutambua taka hatarishi na zisizo hatarishi na ambazo zinaweza kurejelezwa.