Dodoma FM

Wananchi Ihumwa watakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi

7 January 2025, 4:48 pm

Picha ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi .Picha na Polisi Dodoma.

Na Victor Chigwada.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishina msaidizi mwandamizi George Katabazi ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Ihumwa kuonyesha ushrikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu
Wito huo ameutoa wakati akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ambapo amesema katika kuhakikisha wanaongeza nguvu ya suala la usalama wa raia na mali zao jeshi la polisi limeongeza gari kwa ajili ya kufanya doria katika eneo hilo.
Hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kuwafichua wahalifu ili kurahisisha usalama ndani ya kata hiyo

Sauti ya Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma .

Kamanda Katabazi amewaondoa shaka wananchi watakaotoa taarifa kwa jeshi la polisi kuwa zitabaki kuwa siri baina ya jeshi la polisi na mtoa taarifa.

Sauti ya Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma .

Naye Diwani wa Kata ya Ihumwa Edwadi Magawa amekiri uwepo w changamoto ya usalama ndani ya Kata yake inayo sababishwa na mwingiliano wa watu kutoka maeneo tofauti

Sauti ya Edwadi Magawa.