Dodoma FM
Chikopelo watakiwa kutumia mvua za masika kuzalisha mazao mbalimbali
3 January 2025, 3:24 pm
Kijiji cha Chikopelo ni miongoni mwa kijiji kinachopatikana katika Kata ya Chali, ambapo ni miongoni mwa vijiji vilivyotengwa mwaka 1972 kuwa miongoni mwa Kijiji cha Ujamaa. Asili ya wananchi wa Kijiji hicho ni Wagogo.
Na Lilian Leopord.
Wananchi wa Kijiji cha Chikopelo Mkoani Dodoma wameshauriwa kutumia mvua za masika kulima mazao ya aina mbalimbali.
Wito huo umetolewa na Pius Donald Marco ambaye ni Diwani wa Kata ya Chali, ambapo amesema kuwa shughuli kuu ya kijiji hicho ni kilimo na ufugaji na ameongeza kuwa ukame katika kjiji hicho umekuwa kikwazo katika shughuli ya kilimo.
Sanjari na hayo Diwani Pius amebainisha jitihada wanazozifanya katika kukabiliana na changamoto ya ukame.