Dodoma FM

Jafo aanika mafanikio ya Kisarawe

3 January 2025, 2:33 pm

Picha ni Mh. Dkt. Seleman Jafo alipokuwa katika mikutano ya Kata za Msanga na Boga ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa miaka minne.Picha na Seleman Kodima.

Moja ya mafanikio ni ujenzi wa shule nane za sekondari mpya na kuweka miundombinu mipya katika sekondari zote za zamani.

Na Seleman Kodima.
Mbunge wa Kisarawe ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameelezea mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika jimbo hilo kwenye sekta ya elimu, afya, umeme, miundombinu, na maji.

Akizungumza kwenye mikutano ya Kata za Msanga na Boga ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa miaka minne, Dkt. Jafo amesema mafanikio hayo ni pamoja na vijiji vyote 83 vimefikiwa na huduma ya umeme.

Pia, amesema mafanikio mengine ni ujenzi wa shule nane za sekondari mpya na kuweka miundombinu mipya katika sekondari zote za zamani, kujengwa vituo vipya vya afya saba, maboresho makubwa ya Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe pamoja na ujenzi wa zahanati kwenye vijiji mbalimbali.

Picha ni Mh. Dkt. Seleman Jafo alipokuwa katika mikutano ya Kata za Msanga na Boga ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa miaka minne.Picha na Seleman Kodima.