Toto afya kadi kulenga hata mtoto asiyesoma
3 January 2025, 2:13 pm
Na Seleman Kodima.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF ofisi ya Dodoma umesema kipengele kipya cha toto afya kadi kitalenga hata mtoto asiyesoma shule hali itakayomwezesha kusajiliwa katika mfumo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa NHIF Dodoma Fidelis Shauritanga wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema mfumo huo utaweza kusajili mtoto mmoja mmoja, jambo ambalo linatoa nafasi kwa watoto wote kufaidika na huduma za bima ya afya bila vizuizi.
Kwa Upande wake Afisa Mwanachama Mwandamizi kutoka NHIF Bakary Hamduni ameweka bayana utaratibu wa usajili wa mtoto katika mfuko wa taifa ya bima ya Afya.
Hivi karibu Wizara ya Afya imezindua Mfumo wa Uandikishaji Wanachama, Mfumo wa Uchakataji Madai na Vifurushi vipya vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Uzinduzi huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuhakikisha Mifumo ya Serikali inasomana.