Muungano waiomba RUWASA kushughulikia changamoto ya kuharibika kwa miundombinu ya maji
2 January 2025, 6:11 pm
Hili linajiri baada ya hivi karibuni wakala wa usambazaji maji vijijini RUWASA kuiondoa kamata ya maji kijijini hapo.
Na Victor Chigwada.
Kuharibika kwa miundombinu ya maji katika kijiji cha muungano wilayani Chamwino umesababisha wananchi kijiji hicho kuomba kwa mamlaka ya maji vijijini RUWASA kushughulikia changamoto hiyo.
Baadhi ya wananchi wakizungumza na taswira ya habari wamesema hapo awali kamati ilikuwa ikithibiti uharibifu kwa nguvu ukilinganisha na hivi sasa ambapo changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya maji umeongezeka.
Aidha wamesema kuwa adha hiyo imetokana na uhaba wa mafundi kutoka Ruwasa .
kwa Upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho amekiri uwepo wa changamoto ya kupasuka kwa mabomba ya maji hali inayopelekea wananchi kukosa huduma.
Naye Mhandisi wa maji kutoka RUWASA wilaya ya Chamwino Iddi Magoti amesema malalamiko hayo kuondoa kamati za maji ni kwamujibu wa mabadiliko ya sheria na kanuni za usimamizi wa huduma za maji.
Magoti amesema jukumu lao ni kuhusisha wananchi na kuwapa nafasi ya kusimamia miradi ya maji.