Dodoma FM

Tanzania yaendelea kupiga hatua utekezaji mkakati wa Beijing

30 December 2024, 2:11 pm

Picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia nchini TGNP Bi. Lilian Liundi akiongea katika warsha hiyo. Picha na TGNP.

Na Mariam Matundu.

Katika kuelekea miaka thelathini tangu mkutano wa Beijing kufanyika, waandishi wa habari wametakiwa kutumia kalamu zao kuonesha hatua zilizopigwa hapa nchini katika kutekeleza maazimio ya mkutano huo.

Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha wandishi wa habari kutoka maeneo mbalimbali Desemba 28, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi amesema hatua zilizopigwa katika kutetea usawa wa kijinsia si za kubeza.

Sauti ya Bi. Lilian Liundi.
Picha ni mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jinsia nchini TGNP Bi.Lilian Liundi akiongea na waandishi wa habari katika warsha iliyowakutanisha wandishi wa habari kutoka maeneo mbalimbali Dec 28.Picha na TGNP.

Amesema kuwa jinsia ni agenda ya maendeleo na hivyo ni muhimu kutokuachwa kundi nyuma katika mchakato wa kuleta maendeleo katika nchi yoyote duani.

Sauti ya Bi. Lilian Liundi.

Kwa upande wake Laeticia Mukurasi kutoka TGNP amesema ili kufanikiwa katika suala ya usawa wa kijinsia ni muhimu ajenda zake zikabebwa katika dira ya taifa 2050.

waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo kuhusu usawa wa kijinsia na miaka 30 ya Beijing ni kutoka katika mikoa ya Dodoma,Morogoro,Iringa,Mbeya,Manyara,Kilimanjaro,Mtwara,Katavi,Dar es salaam na Kigoma mafunzo yaliyoandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania TGNP.