Mradi wa Elimu jumuishi watekelezwa katika shule 11 Dodoma
23 December 2024, 5:23 pm
Shule zilizoongezeka katika jiji la Dodoma ni shule ya msingi mlezi,shule ya msingi kisasa,shule ya msingi Chang’ombe na shule ya msingi Chinangali.
Na Mariam Matundu.
Mradi wa elimu jumuishi unaotekelezwa na kanisa la Free pentecostal church FPCT mkoani Dodoma umefanikiwa kuongeza shule nne katika halmashauri ya jiji la Dodoma pamoja na shule tano katika halmashauri ya wilaya ya Bahi.
Akizungumza na taswira ya habari mratibu wa mradio huo Jane Mgidange amesema hatua hizo za kuongeza shule zimetokana na mafanikio makuwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa mradi kwa awamu zilizopita.
Aidha amesema ongezo la shule hizo zimelenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu jumuishi .
Nae mwenyekiti wa kikundi cha wazazi wenye watoto wenye ulemavu Mwadawa kiseo amesema kuwa kupitia mradi huo wa elimu jumuishi umewawezesha kuwajengea uelewa na wao kuelimisha kuhusu umuhimu wa watoto wenye ulemavu kupata elimu.
Shule zilizoongezeka katika jiji la Dodoma ni shule ya msingi mlezi,shule ya msingi kisasa,shule ya msingi Chang’ombe na shule ya msingi Chinangali,katika halmashauri ya wilaya ya Bahi zimeongezeka shule ya msingi Bahi misheni,Mkakatika,Mpamantwa barabarani,Ibihwa,Bahi english,na hivyo kufanya jumla ya shule 11 ambazo mradi wa elimu jumuishi unatekelezwa katika Jiji la Dodoma na halmashauri ya wilaya ya Bahi.